JARIDA LA HABARI ZA UM 09 MEI 2023: Lugha ya Kiswahili na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam by UN News Kiswahili published on 2023-05-09T15:03:26Z Jaridani hii leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika jitihada za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendeleza lugha ya Kiswahili kimataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo machafuko nchini Sudan, uzazi salama na maswala ya afya . Mashinani tunakupeleka nchini Ethiopia, kulikoni? 1. Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan waliotawanywa na machafuko mapya ynayoendelea imeongezeka zaidi ya mara mbili wiki iliyopita na sasa kufikia watu 700,000 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. 2. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limezindua ripoti mpya inayoelezea hatua zilizopigwa kuhusu kuokoa maisha wakati wa uzazi na watoto wachanga. 3. Na Tukisalia na masuala ya afya hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Baraza kuu kunafanyika mkutano wa siku mbili wa ulioandaliwa na Baraza Kuu la umoja wa Mataifa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, ukiwaleta Pamoja wadau mbalimbai kuzungumzia masuala muhimu ya afya ikiwemo na huduma za afya kwa wote. 4. Mashinani tutaelekea Tigray nchini Ethiopia kushuhudia kampeni ya chanjo za ugonjwa wa surua na harakati za kusaidia watoto ambao wako hatarini kuathirika na utapiamlo. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu! Genre News & Politics