Jaridani 08 Agosti 2022 na Assumpta Massoi - Unyonyeshaji mtoto maziwa ya Mama by UN News Kiswahili published on 2022-08-08T15:06:31Z Hii leo jaridani tunaanza na habari kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto na tunakwenda Morogoro nchini Tanzania. Kisha tunamulika harakati za FAO kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo ili waweze kupanda mazao msimu huu wa Meher na kisha wavune Oktoba mwaka huu. Makala tunamulika kijana Suzan Yumbe na taasisi yao ya Afya Plus Tanzania na changamoto alizokumbana nazo kuelekea kuanzisha shirika hilo. Mashinani tunasalia Tanzania na ujumbe wa kijana Hussein Meleke kwa vijana wa Kenya wanapokwenda kupiga kwenye uchaguzi mkuu kesho Agosti 9. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics