JARIDANI 09-03-2021 NA FLORA NDUCHA. LEO TUNAYE SAMIA SULUHU HASSAN, MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA by UN News Kiswahili published on 2021-03-09T17:00:18Z Hii leo jaridani Flora Nducha anamulika harakati za kuondokana na ndoa za umri mdogo duniani akimulika mtoto aliyeolewa na mzee huko nchini Bangladesh, kisha anaangazia mpango wa elimu haiwezi kusubiri ambao umepatiwa dola milioni 1 nchini Niger na mwisho ni taarifa kuhusu madereva wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakifanya kazi na Umoja wa Mataifa. Makala tunakwenda Tanzania ambako Paul Siniga, al maaruf Rio Paul anazungumzia jinsi ushiriki wake wa programu ya HeforShe umemsaidia kuwezesha kujenga usawa wa kijinsia nchini Tanzania na usisahau kuna mashinani tukimsikiliza Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Karibu! Genre News & Politics