Makala: Huduma za fedha mtandao zamwondolea mwanafunzi adha ya kufuata fedha benki by UN News Kiswahili published on 2023-05-24T14:41:17Z Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. Ukosefu wa huduma za fedha kimtandao zinakuwa kikwazo kwani wananchi hupoteza muda mwingi benki kusubiria malipo ambayo wangaliweza kuyapokea kupitia simu za kiganjani au rununu. Shuhuda pande zote mbili hizo ni msichana mmoja mkazi wa Cairo nchini Misri kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano duniani, ITU. Genre News & Politics