Jaridani 09 Agosti 2022 na Assumpta Massoi- Vayu Global Health, Vikapu bomba by UN News Kiswahili published on 2022-08-09T15:40:16Z Hii leo jaridani tunaanza na siku ya kimataifa ya watu wa jamii ya asili duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapigia chepuo teknolojia zinazohamishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na wanawake wa jamii ya asili. Kisha tunamulika kifaa cha kupatia hewa ya oksijeni watoto wachanga kilichotengenezwa Kenya na sasa kimepelekwa Ukraine kusaidia hospitali ambako vifaa hivyo ni nadra au havipo. Mashine haitumii umeme! Makala tunamulika kijana Catherine Shembilu kutoka Tanzania na vikapu bomba vinavyotengenezwa na wanawake kwa kutumia majani ya milulu huko Njombe na Iringa, lengo ni kufanikisha SDGs. Mashanani ni kauli ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchaguzi mkuu Kenya. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics