JARIDA LA HABARI ZA UM 22 MEI 2023 NA FLORA NDUCHA by UN News Kiswahili published on 2023-05-22T14:46:08Z Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya ukatili wa kijinsia nchini DRC na msaada wa kibinadamu nchini Myanmar. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka Ureno, kulikoni? 1. Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Bruno Lemarquis amezungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo na kusema vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono dhidi ya wanawake na wasichana kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani nchini DRC vimeongezeka kwa asilimia 37 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, huku akitaka hatua za haraka zichukuliwe ili kurekebisha kinachoendelea. 2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2023 linahitaji dola za Marekani milioni 60 ili kutoa msaada wa chakula cha kuokoa maisha nchini Myanmar kwa watu milioni 2.1 walioathiriwa na majanga mengi na magumu kikiwemo kimbunga Mocha. 3. Makala tunakwenda Morogoro, mashariki mwa Tanzania kusikiliza harakati za shirika lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI) kupitia Mradi wake wa Binti Shupavu, wa kuwajengea Stadi za Maisha wasichana ili kusonga mbele kielimu. 4. Na katika mashinani leo tutakuwa Ureno kwa mtaalam wa sayansi na baolojia ya baharí ambaye pia ni mvuvi na mwanzilishi mwenza wa Ocean alive, Raqel Gaspar akizungumzia umuhimu wa kulinda viumbe wa baharini kama Pomboo na mazingira yao. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu! Genre News & Politics