JARIDA LA HABARI ZA UM 24 MEI 2023 NA FLORA NDUCHA by UN News Kiswahili published on 2023-05-24T14:36:20Z Jaridani leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na ukame uliokithiri katika pembe ya Afrika. Makala tunakupeleka nchini Misri na mashinani nchini DRC, kulikoni? 1. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito SUDAN, UNITAMS amesema bila kujali ni nani anayehusika na janga la kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia wananchi. 2. Hii leo jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwakushirikiana na nchi saba wanachama wa UN wanaendesha tukio la uchangishaji fedha lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni 7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa nchi zilizopo pembe ya Afrika. 3. Makala tunaelekea Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. 4. Katika mashinani na tukiwa tunaelekea siku ya walinda amani duniani leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusikiliza ni kwa jinsi gani tasnia ya michezo ya kuigiza na vipaji vya wenyeji vimesaidia kuzuia unyanyasaji na ukatili wa kingono unaosababishwa na walinda amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu! Genre News & Politics