JARIDA LA HABARI ZA UN 06 JANUARI 2023 NA ANOLD KAYANDA by UN News Kiswahili published on 2023-01-06T15:39:17Z Hii leo jaridani tunnaagazia ripoti ya ILO, na mlo shuleni katika shule za msingi nchini Burundi. Makala tunakupeleka nchini Syria na mashinani nchini Kenya. 1. Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO imepigia chepuo mipango bunifu ya ufanyaji kazi kama ile iliyoanza kutumika kufuatia mlipuko wa janga la COVID-19 ikisema inaweza kuleta manufaa kwa uchumi, biashara na wafanyakazi 2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaripoti kuwa huduma ya chakula katika baadhi ya shule za msingi nchini Burundi tayari inaonesha matokeo chanya kuanzia mahudhurio shuleni na katika upande wa taaluma. 3. Makala tunakupeleka Syria kuona ni kwa vipi misaada inayopitishwa mpakani mwa taifa hilo na Uturuki ina umuhimu mkubwa na hivyo ni vema Baraza la Usalama kuongeza muda wa azimio linalofanikisha mpango huo, azimio ambalo linatarajiwa kumalizika muda wake tarehe 10 mwezi huu. 4. Na katika mashinani tutakwenda Kenya kumsikia mwanafunzi asiyeona lakini ameshika nafasi ya kwanza kwenye shule jumuishi. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! Genre News & Politics