Jaridani 21 Desemba 2021 na Assumpta Massoi- Wakimbizi Cameroon na Zambia by UN News Kiswahili published on 2021-12-21T15:20:34Z Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanza na kufurushwa kwa raia huko Cameroon hususan kutokana na ghasia eneo la kusini-mashariki. Kisha anakwenda Zambia ambako wakimbizi kutoka DRC wameamua kurejea nyumbani kwa hiari kutokana na hali ya usalama kuwa shwari. Na nchini Yemen katikati ya zahma na mizozo familia moja imepata faraha baada ya watoto wao mapacha waliokuwa wameungana kuanzia kifuani hadi tumboni kutenganishwa. Makala tunakwenda Kenya kumulika mpishi wa vyakula vya kiasili aliyepata umaarufu jijini Nairobi na hivyo kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya afya na ustawi. Mashinani tunakukutanisha na shuhuda wa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi nchini Malawi ambaye sasa amepona. Karibu! Genre News & Politics