Jaridani leo 23 Juni 2022 na Leah Mushi - Mada Kwa Kina UNODC Nairobi Kenya by UN News Kiswahili published on 2022-06-23T16:17:26Z Hii leo jaridani Leah Mushi anakuletea habari kwa ufupi na mada kwa kina bila kusahau kujifunza lugha ya Kiswahili. Katika Habari kwa ufupi anamulika unyafuzi na uhitaji wa kusaidia watoto, wito kutoka UNICEF, kisha kikao cha kamati ya WHO cha kubaini iwapo ndui ya nyani au Monkeypox ni dharura ya afya ya umma duniani au la. Na anatamatishia huko Kigali Rwanda ambako Paul Siniga au Rio Paul anaelezea ushiriki wa vijana katika mkutano tangulizi wa CHOGM au Jumuiya ya Madola. Katika mada kwa kina tunamulika mfumo mbadala wa sheria na haki nchini Kenya na katika kujifunza Kiswahili ni methali, Ukipewa Shubiri usichukue Pima. Karibu Genre News & Politics