Jarida 25 julai 2022 na Assumpta Massoi- Kuzama majini, Kajiado, Beni Mavivi by UN News Kiswahili published on 2022-07-25T15:24:20Z Hii leo jaridani tunaanza na siku ya kimataifa ya watu kuzama majini na Umoja wa Mataifa unataka hatua zaidi kuepusha watu kuzama majini kutokana na hali hiyo kuwa sababu inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na ajali. Kisha tunabisha hodi Kenya ambako UNICEF inatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao ipatie kipaumbele hifadhi ya jamii. Makala tunakwenda DRC kuona jinsi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanatoa misaada kwa wanafunzi ili wajifunze Kiswahili na hatimaye wachangie katika kusongesha amani. Mashinani ni tamko la shirika la Umoja wa MAtaifa la afya ulimwenguni , WHO kuhusu maambukizi ya ndui ya nyani au Monkeypox miongoni mwa wanaume mashoga na hatua za kuchukua! Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics