JARIDA 27 07 2022 na Assumpta Massoi - Ghasia DRC tamko la UN na serikali, ubunifu wa Masoud Kipanya by UN News Kiswahili published on 2022-07-27T15:19:31Z Hii leo jaridani tunaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ghasia zinaendelea dhidi ya vituo vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani watatu wa UN wameuawa na watu zaidi ya 61 wamejeruhiwa.. Umoja wa Mataifa umetoa tamko. Kisha kuna hali ya uchumi duniani na makala tunakwenda Tanzania kumulika mbunifu wa gari la kutumia nishati ya umeme, Ali Masoud ‘Kipanya’. Mashinani ni hali ya wanawake nchini Afghanistan, karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics