JARIDA 28 JULAI 2022 Na Assumpta Massoi- Siku ya Homa ya Ini duniani by UN News Kiswahili published on 2022-07-28T15:35:27Z Leo ni siku ya homa ya ini duniani! Hivyo tunakuletea jarida maalum linaloangazia kwa undani aina, maambukizi na vipi mtu anaweza kujikinga asipate homa ya ini ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya wakazi milioni 91 barani Afrika wanaishi nao hususan aina B au C ambayo ni mbaya zaidi. WHO inasema iwapo homa ya ini haitagunduliwa mapema unaweza kupata saratani au kansa ya ini. Je kuna aina ngapi ya homa ya ini? Homa Kali ya ini ni ipi ambayo imegunduliwa sasa? Njia za maambukiz ini zipi? Na nini ufanye uweze kujikinga? Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, na Evarist Mapesa wa Radio washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania wanakuletea kwa kina. Shukrani ikiwa ni kwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es Salaam nchini Tanzania kwa kuratibu mahojiano na maafisa kutoka Wizara ya Afya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO nchini Tanzania. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi. Genre News & Politics