Jaridani na Flora Nducha 07 Septemba 2020 by UN News Kiswahili published on 2020-09-07T15:53:40Z Katika Jarida la Habnari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Katika maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya rangi ya blu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka mshikamano kutokomeza uchafuzi wa hewa -Nchini Pakistan mbinu za kupambana na ugonjwa wa Polio zawa mkombozi mkubwa katika vita dhidi ya corona au COVID-19 ikiwemo miundombinu yake -Waalimu, wanafunzi na wazazi nchini Uganda waelezea changamoto za kusomea nyumbani wakati huu wa janga la corona au COVID-19 -Makala leo inatupeleka Tanzania kumulika athari za COVID-19 katika uhifadhi wa mazingira hasa mbugani -Na mashinani tuko Cote D'voire kuangazia mafunzo ya ujasiliamali yanayotolewa na ILO yanavyosaidia vijana Genre News & Politics