Makala: Chonde chonde Baraza la Usalama ongeza muda wa azimio la kufikisha misaada Syria by UN News Kiswahili published on 2023-01-06T15:26:50Z Ikiwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria ikikariiba kuingia mwaka wa 12, azimio muhimu linalotegemewa katika kufikisha misaada ya dharura nchini humo linatarajiwa kufikia ukomo tarehe 10 mwezi huu wa Januari. Azimio hilo namba 2642 lilikuwa ni la miezi 6 tu ilhali maazimio tangulizi ya aina hiyo ya kuwezesha misaada ya kibinadamu kuingia Syria kupitia mpaka wa Uturiki na Syria upande wa Kaskazini- Magharibi yalikuwa ya mwaka mmoja mmoja. Wito umetolewa na pande mbalimbali duniani kwa azimio hilo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liongezwe muda kwani ndio uhai na tegemeo kubwa kwa wasyria hivi sasa wakati ambao ni msimu wa baridi kali. Je ni kwa kiasi gani azimi hilo linategemewa? Tujiunge basin a Happiness Pallangyo wa Radio washirika UHAI FM kutoka Tabora Tanzania katika makala hii iliyoandaliwa na ofisi ya Umoija wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA. Genre News & Politics