Makala: Iwe malori au baiskeli lazima vifaa vya shule vifikie watoto nchini Burundi by UN News Kiswahili published on 2023-01-09T16:36:56Z Tarehe 24 mwezi huu wa Januari ni siku ya elimu duniani ikimulika mafanikio na changamoto za kufanikisha lengo namba 4 la kufanikisha elimu bora kwa kila mtu kokote aliko. Elimu bora ni pamoja na vifaa ikiwemo madaftari, vitabu na kalamu ambako kwa watoto wengine bado vinasalia kuwa anasa. Mathalani nchini Burundi ambako huko katika baadhi ya maeneo wazazi wanalazimika kufanya vibarua wao na watoto wao ili waweze kumudu madaftari ya shuleni. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake na wadau wamebaini changomoto hiyo na kusambaza vifaa kwenye majimbo sita ya taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. Je ni majimbo yapi? Na mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa na wadau ni yapi? Ungana basi na Edouige Emuresenge, mwandishi wa habari wa Televisheni washirika wetu Mashariki TV, kutoka Burundi katika makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Burundi. Genre News & Politics