Makala: Mkimbizi anayeongoza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Guatemala by UN News Kiswahili published on 2023-01-04T16:56:20Z Mkimbizi Joshua, alipoikimbia nchi yake, kusini mwa Amerika, alilazimika kuingia katika nchi jirani ya Guatemala kusaka hifadhi. Kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi akapata kuunganishwa na shirika lisilo la kiserikali ya FUNDAECO ambako sasa mkimbizi huyu amegeuka kuwa kinara wa kutetea mazingira. Anold Kayanda anasimulia zaidi kupitia makala hii iliyoratibiwa na UNHCR Guatemala. Genre News & Politics