MAKALA: WHO na serikali ya Kenya wasambaza chakula tiba kwa wenye utapiamlo by UN News Kiswahili published on 2023-01-25T14:00:08Z Shirika la Umoja wa mataifa la Afya duniani, WHO kwa ushirikiano na serikali ya Kenya wanasambaza msaada wa chakula tiba cha dharura mahsusi kwa watoto walio na utapia mlo sugu. Watoto hao wanatokea kaunti za Samburu, Turkana na Isiolo ambako ukame na njaa vimepiga kambi. Watoto takriban 10,000 watapata chakula hicho kilicho tayari kuliwa. Thelma Mwadzaya amefuatilia operesheni hiyo na kutuandalia Makala hii. Genre News & Politics