Kupitia asali nimeweza kKupitia asali nimeweza kuwapatia wanawake na vijana shughuli ya kipato by UN News Kiswahili published on 2021-11-23T22:29:10Z Msichana Joreen Wanini wa nchini Kenya, mfanyabiashara ya asali ambaye amefikia hatua ya kuwa chanzo cha ajira kwa watu wengine hususani wanawake na vijana, anawaambia vijana wenzake wawekeze kwenye kilimo na mazao ya kilimo kwani mara zote watu watahitaji chakula na itakuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi katika jamii. Joreen alijiajiri mara tu baada ya kumaliza masomo yake akinunua asali kutoka kwa wakulima wadogowadogo na kuiongezea thamani kwa kuiweka katika vifungashio vizuri kisha kuuza kwa watu wengine wenye uhitaji hasa katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na mfanyabiashara huyo anayechipukia na anayenuia kuboresha maisha ya wanawake na vijana. Genre News & Politics